Leo Mei 29 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, imemuachia huru Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kwa sharti la kwamba, asitoe matamshi ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.
Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa kuwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari alitoa naneno ya uchochezi yenye nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi.
Ilidaiwa kuwa Zitto Kabwe alizungumzia mauaji, yaliyotokea katika Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza mkoani Kigoma ambayo yalisababishwa na vurugu kati ya Polisi na raia.
Ikumbukwe kuwa kwa mara ya kwanza Zitto Kabwe, alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Novemba 2, 2018,