Wivu Wa Mapenzi Wa Sababisha Kifo Cha Mwanamke Shinyanga

Mkazi wa Didia Eliya Paulo Shija (30) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Tuhuma ya Kumuua Mke wake Mariam Juliasi (26) kwa kumchoma na kisu sehemu za shingoni usiku akiwa amelala akimtuhumu kuwa si mwaminifu katika ndoa yao.

Taarifa iliyotolewa Oktoba 11,2020 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Debora Magiligimba imesema kuwa tukio hilo limetokea usiku majira ya Saa saba ambapo Elia alitekeleza mauaji hayo akimtuhumu mkewe anamahusiano na mwanaume mwingine.

“Baada ya kutekeleza mauaji hayo Eliya alijijeruhi kwa kujichoma kwa kisu tumboni na kusababisha utumbo kutoka nje kwa lengo la kujiua kwa sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya,”alisema Magiligimba.

Eliya alikuwa anamtuhumu mke wake kuwa na mahusiano na Mwanaume mwingine ambaye hamjui jina wala sura huku akidai wanawake anaoshirikiana nao kumtafutia mke wake mwanaume ni Lidya Masesa (20 akishirikiana na Mariamu Emmanuel (25) wote wakazi wa Didia.

“Taarifa hizi tumezipata katika ujumbe wa Maandishi ambao Eliya aliuandika katika daftari lilikutwa chumbani kwao,mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga ukisubiri ndugu kwaajili ya Mazishi,”alisema Magiligimba.

Pia Kamanda Magiligimba alitoa wito kwa Wapenzi na Wanandoa kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi na badala yake wapeleke migogoro yao ya ndoa katika ofisi za dawati la jinsia na watoto,viongozi wa dini,na ustawi wa jamii ili kupata suluhisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *