Werder Bremen wachungulia ligi ya daraja la pili baada ya kupoteza 1 – 0

Na katika michezo, Werder Bremen, wanachungulia kandanda la ligi ya daraja la pili ya Bundesliga kwa mara yao ya kwanza kabisa katika historia.

Klabu hiyo inayoshikilia nafasi ya pili kutoka mkia kwenye msimamo wa ligi kuu ya kandanda Ujerumani, ilipoteza mechi yake ya jana kwa kufungwa bao moja kwa nunge na VfL Wolfsburg.

Schalke 04 nayo ilijiwekea rekodi yake mbovu ya kutopata ushindi katika mechi 12 mfululizo, kwa kutoka sare ya 1 – 1 na Union Berlin.

FC Augsburg walitoka sare ya 1 – 1 na FC Köln katika mechi ya mwisho jana jioni. Katika michezo hiyo, wachezaji waliendelea kuonyesha mshikamano na maandamano yanayoendelea ulimwenguni yakianzia Marekani ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *