Waziri Mkuu wa zamani wa Lesotho ‘aliwapa majambazi kumuua mke wake wa zamani”

Polisi nchini Lesotho wamesma kuwa wana ushaidi kwamba aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Thomas Thabane na mke wake wa sasa Maesaiah walilipa majambazi kumuua mke wazamani wa Bw.Thabane mwaka 2017.

Lipolelo Thabane alipigwa risasi na kuuawa usiku wa kuamkia siku ya kuapishwa kwa Bw. Thabane kuwa waziri mkuu.

Taarifa ya polisi katika moja ya stakabadhi ziliyowasilishwa mbele ya Mahakama Kuu ya Maseru High inapinga ombi la Bi.Thabane kutaka achiliwe kwa dhamana.

Mke huyo wa sasa wa Thabane, ambaye anakabiliwa na mashitaka ya mauaji, amekuwa akizuiliwa tangu wiki iliyopita.

Mawakili wake wanataka aachiliwe kwa dhamana ili akamhudumie mumewe mgonjwa.

Alipinga mashitaka dhidi yake.

Bw. Thabane – ambaye amekana kuhusika na mauaji hayo – alilazimika kujiuzulu mwezi uliyopita kutokana na madai sakata hayo ya mauaji.
Bado hajafunguliwa mashitaka, lakini stakabadhi za polisi zinadai kuwa aliwaonesha majambazi nyumbani kwa mke wake wa zamani.

Polisi pia wanasema waziri mkuu huyo wa zamani na mke wake walidaiwa kuwalipa majambazi kima cha dola elfu 180 sawa na (£142,000) – ambayo ilikuwa ilipwe kwa awamu.

Dola elfu 24 tayari zilikuwa zimelipwa, kwa mujibu wa stakabadhi hizo zilizo wasilishwa mahakamani chini ya kiapo.

Mmoja wa majambazi hao anatarajiwa kutoa ushahidi kwa niaba ya taifa.
Bi Lipolelo alikua tayari ameshinda kesi ya kutambuliwa kama mke wa kwanza wa waziri mkuu badala ya Maesaiah.

Maesaiah akiandamana na bwana Thabane wakati alipokuwa akila kiapo baada ya kifo cha mkewe wa kwanza.

Miezi miwili baadaye yeye na bwana Thabane walioana katika sherehe ya kikatoliki iliofanyika katika uwanja wa Maseru uliojaa.

Kwa mujibu wa polisi, Bw. na Bi. Thabane walitaka kumuua, Lipolelo, ili mke wake wa sasa apate nafasi ya kuwa mama taifa.

Muda mfupi kabla ya kifo chake, Lipolelo Thabane alishinda kesi mahakamani ya kuthibitisha kuwa yeye ndiye mama taifa halisi wa Lesotho – na kwamba licha ya kuwa katika ya mgogoro wa kesi ya talaka – alistahili kulipwa mafao yanayotokana na wadhifa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *