Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akiwa ziarani nchini Afrika kusini amejibu kuhusiana na madai ya RaisTrump wa Marekani kwamba yeye Rais Trump ndiye aliyestahiki kupata tuzo ya Nobel.
Abiy alisema kuwaambia wanahabari waliomuuliza juu ya suala hilo,
” Sifahamu ni vigezo gani vinatumika kumchagua mtu wa kumpatia tuzo ya “.
Trump katika mkutano wa kampeni huko Ohio alisema ,
“ Nilifanya makubaliano Fulani, Nikaiokoa nchi moja. Lakini nasikia kwamba Kiongozi wan chi hiyo amepewa tuzo ya amani ya Nobel kwa kuiokoa nchi hiyo.”
Pamoja na kwamba Rais wa Marekani hakutaja jina la Ethiopia wala la Abiy waziwazi, lakini kauli zake hizo zilipingwa vikali nchini Ethiopia.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema Rais Trump alikuwa akizungumzia mgogoro baina ya Misri na Ethiopia uliotokana na mazungumz