Waumini wa Dini ya Kiisilam Wilayani Kahama wameelekezwa kuendelea kufuata maelekezo ya kujikinga na Corona

Katika kupambana na janga la virusi vya  Corona, Waumini wa dini ya kiisilam wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameelekezwa kuendelea kuzingatia namna Bora ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kuzingatia  maelekezo yaliyotolewa na serikali pamoja na baraza kuu la waislam Tanzania (Bwakata).

Kauli hiyo imetolewa Leo mjini Kahama na Shekh wa walaya ya Kahama, ALHAJI OMARI DAMKA wakati akipokea msaada wa vitu mbalimbali Kwaajili ya mfungo wa mwezi mtUkufu wa ramadhani iliyotolewa na halmashauri ya mji wa Kahama.

Amesema tangu janga Hilo liingie nchini, wamekuwa wakiwaelekeza  waumini namna ya kuchukua tahadhari ikiwamo kuvaa Barakoa, kunawa kwa sabuni na maji tiririka,  na kukaa kwa kupeana nafasi.

Awali Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Kahama ANDERSON MSUMBA amesema msaada huo Wameutoa kwaajili ya kuwasaidia waislam  ili kusherehekea vema siku kuu ya EID.

Msaada uliotolewa ni Mchele, kg 1000, unga wa ngano kg 100,  Sukari Kg 200, mafuta ya kula Lita 200, Maharage kg 442 na tambi boksi 40,  vyenye tathani ya zaidi ya shilingi Milioni tano ambapo Shehe DAMKA ameelekeza kugawiwa kwa watu wenye uhitaji, Kama vile, yatima, wajane na wazee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *