Watu 41 wamefariki Dunia kufuatia mlipuko wa Virusi vya Corona China

Ripoti mpya kutoka China zinasema Watu 41 wamefariki Dunia na wengine 1287 wakithibitika kupata madhara kufuatia mlipuko wa Virusi vya Corona

China imeifunga sehemu ya ukuta wake maarufu na kusitisha safari za umma katika Miji kumi na Watu wameonekana wakiwa wamevaa mask ikiaminika inasaidia kujikinga.

Tayari virusi hivyo vimesambaa ambapo Thailand wamebainika wagonjwa watano, Vietnam (2) Singapore (3), Japan(2), Korea Kusini(2), Taiwan(3), Nepal(1), Ufaransa(3) na Marekani(3).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *