Watu 12 wauawa katika shambulizi Mali

Karibu watu 12 wameuawa katika shambulizi lililofanywa kwenye vijiji kadhaa vya katikati ya Mali, ikiwa ni machafuko ya karibuni kabisa kuikumba nchi hiyo iliyoharibiwa kwa vita.

Watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki walivamia vijiji kadhaa karibu na mji wa Bandiagara katika jimbo la katikati ya Mali la Mopti, kwa mujibu wa jamaa wa mmoja waathiriwa na ripoti ya ndani ya Umoja wa Mataifa. Ali Dolo, Meya wa eneo hilo amesema kinachowauwa ni vita na wala sio virusi vya corona akiongeza kuwa wavamizi hao walichukua ng’ombe 500.

Mali inapambana kudhibiti uasi wa itikadi kali ulioanza 2012, na ambao umesababisha vifo vya maelfu ya wanajeshi na raia tangu wakati huo.

Licha ya uwepo wa maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Mataifa, mzozo huo umelikumba eneo la kati la nchi hiyo na kusambaa katika nchi jirani Burkina Faso na Niger.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *