Waponda kokoto kahama waiomba serikali kutowahamisha

KAHAMA

Waponda kokoto wa mlima wa Noremko  wa mtaa wa shunu katika halmashauri ya kahama mji mkaoni shinyanga wameiomba serikali ya mtaa wa shunu wasiwaondoe katika eneo hilo na waendelee na shughuli za kuponda  kokoto ili waweze kujikumwamua kiuchumi.

Haya yamesemwa  na baadhi waponda kokoto wakati   wakizungumza na kahama fm kwa nyakati tofauti wamesema biashara hiyo wanaitegemea kwa ajili ya kulisha familia zao, kulipa mikopo wanayodaiwa na kuwasomesha watoto wao.

Hata hivyo, wamesema hawataza kuondoka eneo hilo kwa sababu hawana sehemu nyingine ya kwenda na kumtaka mwenyekiti wa mtaa wa shunu kusitisha mpango huo na kuwaonea huruma kwa maana wanategemewa na familia zao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa waponda kokoto wa mlima huo VICENT CHARLES amesema hawataweza kuondoka katika milima huo na hawezi kumahama isipokuwa waachwe waendelee na shughuli za maendeleo katika eneo hilo.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa shunu  JAPHET KALIU akifafanua juu ya taarifa hizo si za kweli na kuwataka waponda kokoto wa eneo hilo waendelee na shughuli za za kila siku na endopa kutakuwa na madiliko wataarifimwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *