Wanawake wasuasua uchaguzi mkuu

Imeelezwa kuwa kati ya wagombea wa vyama 15 walioteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wanawake 7 waliweza kujitokeza.

Hayo yameelezwa na na Jaji mstaafu,Thomas Mihayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa Mara.

Shayo alisema kuwa jumla ya wagombea wa vyama 15 walioteuliwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi wanawake wawili waliweza kujitokeza kugombea nafasi ya kiti cha urais huku wanawake watano walijitokeza kugombea nafasi ya makamu wa Rais.

Shayo alitumia nafasi hiyo kuwataka wadau wa uchaguzi kwenda kutoa elimu ya uchaguzi kwenye maeneowanayotoka ili elimu kuwafikia wapiga kuna na kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.

“Kwa upande wa elimu ya mpiga kura Tume chini ya kifungu cha 4(c)cha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343 imepewa mamlaka ya kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima kuratibu na kusimamia Asasi zinazotoa elimu,hiyo kwa sasa Tume inaendelea kutoa elimu ya mpiga kura kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya wadau kama inavyofanya sasa kutumia vyombo vya habari machapisho sanaa magari ya matangazokushiriki matamasha na maonyesho kama hivin leo ambapo tunaomba elimu hii kuwafikishia walio katika maeneo yenu”alisema Shayo.

Kwa upande wake Wilson Mahera ambaye ni mkurugenzi wa uchaguzi aliwataka wanasiasa na mashabiki kuzingatia sheria na taratibu za Tume ya uchaguzi zilizopo ilikuepuka migogoro

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *