Wanawake wanaongoza kudhalilishwa mtandaoni

Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imesema Wanawake wanaongoza kwa kudhalilishwa mitandaoni Nchini Tanzania kutokana na kuwa na tabia za kupiga picha zenye utata na kuzituma mitandaoni pamoja na kutumia simu za wapenzi wao kupiga picha za utupu.

Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria na Masharti ya Leseni, Dr. Philip Filikunjombe amesema takwimu hizo ni kwa mujibu wa kesi wanazopokea katika Mamlaka hiyo ambazo nyingi zinawahusu Wanawake kudhalilishwa mitandaoni.

Ameeleza kuwa, Waathirika wa matukio hayo wanapofika TCRA kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya waliofanya uhalifu huo huwa inabainika kwamba Wahusika walizipiga picha hizo wenyewe.

Kwa kumalizia, amesema suala hili pia linachangiwa na ugawaji wa password kwa Watu wa karibu au Wapenzi wao, kingine ni tabia ya kupiga picha za utupu au kuzipokea na kuzihifadhi kwenye simu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *