WANANCHI JOMU WANUFAIKA NA PETS

Wananchi wa kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya shinyanga vijijini mkoani Shinyanga wamenufaika na shughuli za mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma ( PETS).
Wakizungumza katika mkutano wa kuonyesha matokea yaliyofikiwa na wananchi kupitia mradi wa PETS katika kijiji cha jomu baadhi ya Wananchi wa kijiji hicho wamesema kwa sasa wana mwamko mkubwa wa kimaendeleo ikiwemo kuwapeleka shuleni watoto wenye ulemavu tofauti na awali.
Mwenyekiti wa kijiji cha jomu JOHN MASELE amesema kupitia elimu jumuishi iliyotolewa na mradi wa PETS wamepeleka shuleni wanafunzi 10 wenye ulemavu wakike 4 na kiume 6 na kujenga chumba kimoja cha darasa kwa ajili ya watoto hao.
Amesema kuwa kabla ya ujio wa PETS wananchi waliamini kwamba watoto wenye ulemavu hawakupaswa kwenda shule lakini baada ya ujio wa mradi huu wameona umuhimu wa kupeleka watoto wenye ulemavu shuleni.
Ameongeza kuwa jitihada zinaendela kuhakikisha wanatengeneza miundominu rafiki kwa watoto hao ikiwemo kuwapatia vifaa vya kusomea.

Mwenyekiti wa chama cha wasioona mkoani Shinyanga MICHAEL NKANJIWA amesema matunda yaliyopatikana kupitia mradi huu yasiishie katika kijiji cha Jomu pekee kwani utaongeza uwajibikaji kwa viongozi wa umma.
Mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma(PETS) ni mradi endelevu chini ya ufadhili wa shirika la foundation for civil society unaotekelezwa katika mkoa wa Shinyanga kwa baadhi ya meneo ya manispaa ya Kahama na wilaya ya Shinyanga vijijini huku lengo likiwa ni ufuatiliaji wa rasilimali za umma kwa ujumla zilizotengwa kwa ajili ya elimu maalumu na jumuishi kwa watu wenye ulemavu..

CHRISTNA CHRISTIAN

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *