Wanamgambo 275 wa Taliban wajisalimisha Afghanistan

Wanamgambo 275 wa kundi la Taliban wameripotiwa kuacha silaha na kujisalimisha kwa serikali katika mikoa ya Sar-i Pul na Balkh kaskazini mwa Afghanistan.
Naibu Msemaji wa Wizara ya Ulinzi Fawad Aman alitoa maelezo na kuelezea kwamba wanamgambo 150 wa kundi la Taliban walijisalimisha serikalini wakiwa na silaha zao mjini Balhab mkoani Sar-i Pul.

Aman aliongezea kusema kuwa miongoni mwa wanamgambo hao, kulikuwa na makamanda 15 wa kundi la Taliban.

Kwingineko katika mji wa Charkent mkoani Belh, wanamgambo 125 walijisalimisha serikalini na kuahidi kwamba hawatojihusisha tena na Taliban wala kupigana.

Kundi la Taliban halijatoa maelezo yoyote kuhusiana na tukio hilo.

Kwa miaka mingi kundi la Taliban na wajumbe wa serikali ya Afghanistan wamekuwa wakiendesha mchakato wa kusitisha mapigano katika mji mkuu wa Doha nchini Qatar. Kitendo cha wanamgambo wa Taliban kujisalimisha makundi kwa makundi hasa kwa kipindi hiki kimekuwa cha kushangaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *