Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini,Wameshauriwa kuweka Sera ya Usalama wa mawasiliano katika vituo vyao.

Ushauri umetolewa kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuweka Sera ya usalama wa mawasiliano katika vituo vyao ili kulinda kazi za kihabari na kutunza siri za ofisi.

Hayo yamesemwa leo Visiwani Zanzibar na Mkufunzi kutoka Shirika la UNESCO Leonard Kisenha katika mafunzo ya TEHEMA kuhusu usalama wa mfumo wa mawasiliano.

Kisenha amesema kuwa kupitia mifumo ya mitandao na internet kuna Virusi vinavyoweza kuharibu kazi zilizohifadhiwa kwenye mifumo ya Computer na wakati mwingine kusambaa kwa taarifa za siri kunakosababishwa na udukuzi.

Sambamba na hayo Kisenha amewataka waandishi wa habari kuacha kutumia Internet za Bure (Wi-fi) kufanya mambo ya Muhimu kuhusu kazi zao za kihabari kwani kuna uwezekano mkubwa wa kudukuliwa na kusambaa kwa kazi zao.

Nao baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo Hussein Ayubu kutoka Radio Uvinza Kigoma na Amina Mrisho kutoka Radio Pambazuko Morogoro wameishukuru UNESCO kwa mafunzo hayo kwani yatawasaidia kuongeza usalama katika kazi zao za kila siku.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na utamaduni (UNESCO) limetoa Elimu ya mafunzo ya TEHAMA kwa Radio ishirini na tano za kijamii kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *