Waliofariki kwa corona China wafikia 2,118

Idadi ya waliofariki kutokana na virusi vya corona China imeongezeka na kufikia Watu 2118, huku uwezekano wa vifo kuongezeka ukiwa ni mkubwa, walioathirika na virusi hivyo mpaka sasa ni 74,576 hii ni kwa China pekee.

Wagonjwa 11,864 wa corona wako mahututi huku wagonjwa waliotibiwa Hospitali na kuruhusiwa wakiongezeka na kufikia 16,155.

Takwimu za jana idadi ya waliofariki kwa corona ilikuwa Watu 2004, walioathirika na virusi hivyo  walikuwa 74,185 hii ni kwa China pekee, wagonjwa 11,977 waliripotiwa kuwa mahututi, ambapo wagonjwa ambao walitibiwa Hospitali na kuruhusiwa walikuwa 14,376

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *