Wakulima wa Tumbaku Tabora waiomba Petrobena kuwapelekea mbolea za Mahindi.

Wakulima wa Tumbaku mkoani Tabora wameiomba kampuni ya Usambazaji wa Pembejeo ya Petrobena kuwasambazia mbolea ya UREA  kwa ajili ya kilimo cha mahindi kwani zao hilo linawasaidia kupata chakula.

Wakiongea katika mkutano wa mkuu wa 27 wa chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi (WETCU) baadhi ya wakulima wamesema kuwa uzalishaji wa mahindi ni mdogo hali inayosababisha familia nyingi kukosa chakula cha uhakika.

Wameongeza kuwa kilimo cha Tumbaku kinahitaji nguvu kazi na nguvukazi inahitaji Chakula hivyo kukosa mbolea ya mahindi kunasababisha nguvu kazi hiyo kushindwa kufanya uzalishaji mzuri wa Tumbaku.

Katika mapendekezo yao wakulima hao wameomba kupatiwa mifuko miwili ya UREA kwa heka moja na kwamba hali hiyo itasaidia kupata mahindi mengi ambayo yatasaidia kwa chakula katika familia zao.

Katika hatua nyingine wakulima hao wameomba kufanyiwa tathimini ya idadi ya heka za mahindi wanazolima kwa kila kaya kama wanayofanyiwa kwenye Tumbaku ili kujua idadi za mbolea ambazo watakopeshwa ili kuinua zao hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *