Wakazi wa Meatu Mkoani Simiyu walia na Ukosefu wa Maji safi baada ya Chanzo cha maji kukauka.

Na Anitha Balingilaki,Simiyu

Wakazi wa mji wa Mwanhuzi wilayani Meatu mkoani Simiyu wamekumbwa na tatizo la ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kutokana na chanzo walichokuwa wanakitegemea kukauka.

Hali hiyo inatokana na wilaya hiyo kukumbwa na ukame sambamba na bwawa la Mwanyahina kujaa tope  na hivyo kupelekea bwawa hilo   ambalo wamekuwa wakilitegemea kukauka.
Baadhi ya wananchi wa mji huo wameuomba uongozi wa wilayani  hiyo kuwasaidia kutatua tatizo hilo kwa kuwa bei ya maji imepanda kwa kiasi kikubwa.

Mkuu wa wilaya hiyo Dokta JOSEPH CHILONGANI amesema tayari wameshachukua hatua za kukabiliana na changamoto hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *