Waislamu wa Ki-ibadhi Kahama kwa Kushirikiana na Waislamu wa Madhehebu ya Ki-Sunni waungana kumuombea Mfalme Qaboos Bin Said Al-Said.

WAUMINI wa dini ya Kislamu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,wamemuomba Mfalme aliyepo sasa wa nchi ya Omani Mfalme Haitham Bin Tarik Taimur Al-Said kufuata nyazo za kuzisadia nchi za afrika kama alivyokuwa akifanya mfalme aliyetangulia Qaboos Bin Said Al-Said.

 

Wito huo ulitolewa jana na Shekhe wa Wilaya Omari Damka katika idala maalumu ya kumuombe aliyekuwa Mfalmae wa nchi ya Omani Qaboos Bin Said Al-Said iliyofanyika katika Masjid ya Al-waahab iliyopo kata ya Nyasubi mjini hapa.

 

Alisema kuwa,Mfalme Qaboos Bin Said Al-Said aliijenga nchi ya omani kwa amani bila kumwaga damu ikiwa ni pamoja na kuzisaidia nchi za Afrika kwa kujenga Msikiti sehemu ambazo hazina nyumba za ibada na kuchimba visima virefu vya maji.

Aidha Damka alisema kuwa,akinamama wanaoishi pembezo mwa miji walikuwa wanatembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji safi na salama lakini kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania chini ya Jumuiya Istiqaama Intertional Muslim Community wamweza kujenga visma virefu vya maji.

 

“Hakuna nchi ya afrika ambayo Mfalme Qaboos Bin Said Al-Said kwa kushirikiana na Istiqaama Intertional Muslim Community hawajajenga msikiti,shule wa kuchimba visima vya maji,Tumuombne Mungu amfanye Mfaklme aliyeko sasa amefuate nyao hizo kama njia ya kumuenzi”Alisema Damka.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Istiqaama Mohamed Issa amewataka wananchi Wilayani kahama kuvitunza visima vilivyochimbwa maeneo mbalimbali yaliyekuwa na changamoto ya maji ili visije vikaharibika kabla havijawanufaisha na wengine wenye changamoto ya maji safi na salama.

 

Pia aliwaka wananchi wasiokuwa waislamu na waslamu kumuombea Mfalme aliyepo sasa Haitham Bin Tarik Taimur Al-Said aendelee kuzisaidia nchi za afrika kwa utajili alionao kwa kujenga nyumba za ibada,shule na kuendelea kuchimba visima vya maji maeneo yenye changamoto ya maji.

 

Hata hivyo alisema kuwa,kwa Mkoa wa Shinyanga,Halmashauri ya Msalala inaongoza kuwa na Visima hivyo vya maji nakuongeza katika miradi iliyoanzishwa na ile ambayo bado haijakamilika watahakikisha wanaikamilka kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi.

 

Nae Zuwena Juma aliiomba Jumuiya ya Istiqaama kujenga taasisi za elimu kwenye maeneo yasiyokuwa na shule ili kuwapunguzia adha wanafunzi kutembea umbali mrefu kutafuta elimu na hii itasaidia wanafunzi hasa wa kike kutokatisha masomo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *