Waislamu wa Ki-Ibadhi Kahama Kwa Kushirikiana na Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama ya nchini Oman watoa msaada kwa wagonjwa.

Mashirika yasiyo ya kiserikali,Taasisi na Watu binafsi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameombwa kujitokeza kuwasaidia wagonjwa wasiojiweza mahospitalini kwani baadhi yao hawana ndugu wakuweza kuwasaidia.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Masjid Al-wahabu Mohamed Issa Hilaly Al-Habsy wakati akikabidhi msaada kwa niaba ya jumuiya ya Internatioanl istiqumaa Muslim Community  ya nchini Oman katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Al-Habsy amesema kuwa ukimsaidia mtu mwenye matatizo mtu Yule akashukuru kwa ulichotoa hivyo mwenyezi Mungu atakujulia mema katika shughuli zako na familia yako.

Kwa upande wake katibu wa Masjid Al-wahabu Shehe Ahmed Haroun Al-Nuby amesema kuwa msaada huo wameulenga sana kwa watu ambao hawajiwezi,na kwamba wameona kuna umuhimu wa kuwasaidia wanyonge.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mganga mkuu, Mganga wa zamu katika hospitali hiyo Adam Masaguda ameishukuru jumuiya ya kiislamu ya Istiqamaa kwa msaada huo na kuongeza kuwa katika hospitali hiyo kuna wagonjwa wengi wanaohitaji msaada kwani kuna wengine hawana ndugu .

Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa na waangalizi wa wagonjwa waliopata msaada huo wameishukuru jumuiya ya Internatioanl istiqumaa Muslim Community  ya nchini Oman kwa msaada huo na kwamba imewapunguzia gharama za matumizi kwa kiasi kikubwa.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *