Wafungwa 7 wafariki katika ghasia zilizozuka katika gereza nchini Mexico

Wafungwa  7 wafariki na wengine  9 wajeruhiwa katika ghasia zilizotokea katika gereza moja nchini Mexico.

Ghasia zilizotokea katika gereza moja nchini Mexico zimepelekea wafungwa  7 kufariki na wengine  9 wamejeruhiwa vikali.

GHasia hizo zimetokea katika gereza  lenye ulinzi mkali  katika jimbo la Puente Grande.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na  vyombo vya habari nchini Mexico, wafungwa walishambulia kwa silaha za moto na visu na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.

Hali imerejea kuwa shwari  baada ya  maafisa magaereza kuingilia kati.

Uchunguzi umeanzishwa kubaini sababu na ghasia hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *