Waandishi wa Radio 25 za kijamii wanolewa Dodoma,Lengo kuzitambua jamii zinazowasikiliza na kuwafikia kirahisi.

Waandishi wa Habari kutoka katika Redio za kijamii zaidi ya 25 wapatiwa mafunzo ya Utafiri wa wasikilizaji

Mafunzo hayo yanayoendelea kwa siku tano yamewezeshwa na Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO, yanafanyika katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Akizungumzia lengo la mafunzo hayo Bw: Marko Gedion kutoka UNESCO amesema lengo ni kuwajengea uwezo waandishi na watangazaji wa Redio za kijamii ili kutambua jamii ya wasikilizaji wanayohiudumia na kurahisisha ushiriki wao katika vipindi vya Redio.

Kwa Upande wake Mkufunzi wa Mafunzo hayo Bw: Samwel Muthoka kutoka Ipsos Tanzania limited amewataka washiriki wa Mafunzo hayo kushiriki kikamilifu ili kwenda kuboresha vipindi vya redio na kuendelea kuongeza idadi ya wasikilizaji.

Bw: Muthoka ameongeza kuwa Redio bado ni chombo kinacho aminika na kusikilizwa zaidi na watu wengi ukilinganisha na vyombo vingine vya habari kwa kufikia sehemu kubwa ya jamii hasa vijijini.

Akizungunza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo Bw: Amua Rushita kutoka Redio jamii FM , amesema kuwa mafunzo haya yatasaidia Redio za kijamii kutambua usikivu wa redio na namna ya kuboresha mahudhui yanaopendwa na watu wengi zaidi.

Wanaopata mafunzo hayo ya siku tano ni waandishi wa habari 25 kutoka Redio 25 za kijamii Tanzania bara na Zanzibar ikiwa ni awamu ya pili kufanyika jijini Dodoma

CREDIT: MATHIAS TOOKO
(LOLIONDO FMA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *