Waandishi wa habari watakiwa kuacha kuandika habari za Propaganda kuelekea uchaguzi mkuu 2020.

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuacha kuandika habari za Propaganda kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 ili kuepeuka kuleta machafuko nchini kwa kutumiwa na vyama vya  siasa.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na mwanahabri Mkogwe Attilio Tagalile katika kikao kazi cha Siku moja kuhusu usalama wa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu 2020 yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Policy Forum.

Tagalile amewataka waandishi kuandika habari zenye mashiko na zenye ukweli katika jamii na kuacha kuandika habari za uongo zinazotolewa na wanasiasa kwa lengo la kuvuta wapiga kura ili wawapigie kura kwa kuamini kuwa kinachosemwa ni sahihi kumbe si kweli.

Ameongeza kuwa jamii inaviamiani sana vyombo vya habari hivyo kuandika habari zisizo na ukweli kutasababisha vurugu na kuleta mgawanyiko mkubwa katika jamii kama ilivyotokea Rwanda mwaka 1994.

Katika hatua nyingineTagalile amewataka wanahabari kuacha kutumia vyombo vya usafafiri vya wanasiasa na kupokea posho wakati wa Uchaguzi kwani kwa kufanya hivyo kutawafanya waandike habari za upendeleo kwa chama kimoja.

Nao baadhi ya waandishi wa habari za radio za kijamii ambao wameshiriki katika kikao kazi hicho wamelishukuru shirika la Policy Forum kwa kuandaa kikao kazi hicho na kwamba elimu waliyopata itawasaidia katika kuandika habari zenye weledi kuelekea uchaguzi mkuu 2020.

Kikao kazi hicho cha Siku moja kilichofanyika katika Hotel ya Seascape jijini Dar es salaam kimeshirikisha Radio nne za kijamii ambazo ni Kahama Fm kutoka Shinyanga,Mashujaa Fm ya Lindi,Nuru Fm ya Iringa na Safari Fm ya Mtwara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *