Waandishi nchini wametakiwa Kutumia TEHAMA kuleta mabadiliko katika Jamii zinazowazunguka.

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuinua kiwango cha Elimu,Biashara,Ajira pamoja na utunzaji wa mazingira katika jamii zinazowazunguka.
Wito huo umetolewa leo na Mkufunzi a TEHAMA kutoka UNESCO Mdegela Ajuaye katika mafunzo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA yalionza leo Visiwani Zanzibar yakishirikisha radio Ishirini na Tano za kijamii kutoka Tanzania Bara na visiwani.
Ajuaye Amesema kuwa Matumizi ya TEHAMA yana mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa katika nyanja mbali mbali na kwamba waandishi wa habari wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kutumia teknolojia hiyo katika kazi zao.
Sambamba na hayo Ajuaye amewataka wana habari kuacha kutumia TEHAMA kwa mambo yasiyo na maslahi na badala yake wawe wabunifu katika kuisaidia jamii kuleta mabadiliko hususan katika sekta ya Kilimo na utunzaji wa mazingira.
Nao baadhi ya wanahabari Hafidhi Ally kutoka Nuru Fm Iringa na Fatma Saleh kutoka Radio Jamii Mtegani Unguja wameshukuru UNESCO kuwapatia mafunzo hayo kwani yatawasaidia kuifikia jamii kwa urahisi na kujua njia za kisasa za kutunza vipindi na taarifa mbalimbali za radio.
Kwa mujibu wa mratibu wa Mafunzo hayo kutoka shirika la UNESCO Getruda John amesema jumla ya Radio 25 za kijamii ndizo zitakazonufaika na mafunzo hayo ishirini na moja kutoka bara na radio nne kutoka Zznazibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *