Waandamanaji wa Uingereza wanaopinga ubaguzi wa rangi baada ya kutokea kifo cha #GeorgeFloyd wameivunja na kuitupa kwenye maji sanamu ya aliyekuwa mfanyabiashara ya utumwa iliyoko mjini Bristol
Sanamu ya Edward Colston ilikuwepo tangu mwaka 1895. Watu walipitisha chagizo la kuiondoa sanamu hiyo kwa kuwa ilikuwa inabeba historia mbaya, hivyo katika maandamano hayo waandamanaji waliitupa sanamu hiyo
Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yameendelea kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo London, Rome, Madrid, Warsaw, Sydney na Hongkong huku waandamanaji wakiwa na ujumbe usemao ‘#BlackLivesMatter’
Katika maeneo mengi, waandamanaji wameonekana kutojali uwepo wa #CoronaVirus kwa kutoachiana nafasi inayoshauriwa kati ya mtu na mtu. Pia ni wachache kati yao ambao huvaa barakoa