Waandamanaji kadhaa wakamatwa nchini Belarus

Watu kadhaa wamekamatwa nchini Belarus jana Jumapili wakati wa maandamano ya umma dhidi ya rais Alexander Lukashenko ambaye alishinda muhula wa sita katika uchaguzi unaozingatiwa na wengi kuwa uliandamwa na wizi wa kura
Mamia kwa maelfu ya watu walikusanyika kwa wiki ya kumi mfululizo kwenye mji mkuu wa Belarus, Minsk, kushinikiza kujiuzulu kwa rais Lukashenko aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 26.

Kundi la haki za kiraia liitwalo Viasna limechapisha kwenye tovuti yake orodha ya waandamanaji wanaofikia 300 ambao inasema walikamatwa na voymbo vya dola kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Asasi ya Viasna inakadiria kuwa kiasi watu 100,000 walishiriki maandamnao ya jana ambayo yalitawanywa na polisi waliotumia magari ya maji ya kuwasha, mabomu ya kutoa machozi pamoja na virungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *