Vijana wawili wa miaka 14 mbaroni kwa ubakaji

Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linawashikilia vijana wawili Boazi Shija (14)na Jakaya John(14) kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye miaka Sita(jina limehifadhiwa).Watuhumiwa hao ni wakazi wa Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba,amesema kuwa vijana hao walimlaghai mtoto huyo kwa pipi na kumpa hela kisha kumpeleka Kichakani karibu na eneo analoishi na wazazi wake kisha kisha kumfanyia unyama huo.

Hata hivyo jeshi la Polisi limesema kuwa watawafikisha mahakamani watuhumiwa hao mara baada ya upelelezi kukamilika na hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *