Urambo yatoa mikopo ya milioni 167.2 kwa vikundi 27

HALMASHAURI ya Wilaya ya Urambo imetoa mikopo ya kiasi cha shilingi milioni 167.2 kwa vikundi 27 vya wajasiriamali toka Julai mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Baraka Zikatimu wakati akiwasilisha jana taarifa ya shughuli zilizofanyika katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Novemba mwaka huu kwenye kikao cha Baraza jipya la Madiwani.

Alisema Wajasiriamali waliofanikiwa kupata fedha hizo ni vikundi 11 vya wanawake, vijana 13 na walemavu vikundi 3.

Zikatimu alisema vikundi vya wanawake vilipatiwa shilingi milioni 70, vijana walipatiwa milioni 82.2 na watu wenye ulemavu walipatiwa shilingi milioni 15.

Alisema katika fedha hizo walikopesha vikundi kiasi cha shilingi milioni 65 zinatokana na fedha za mwaka uliopita wa fedha wa 2019/20 na zilizobaki zinatokana marejesho na zile za asilimai 10 ya makusanyo ya mwaka wa fedha unaoendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati alisema ni vema Halmashauri zinapotoa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana , wanawake na walemavu zikatoa fedha nyingi ambazo zitaleta matokeo makubwa na maendeleo katika maisha ya wakopaji.

Alisema pia Halmashauri zijielekea kuviwezesha mikopo ya vifaa ambao vinaweza kuwasaidia kuanzia viwanda vidogo vya kuzalishia bidhaa mbalimbali.

Dkt. Sengati alisema hatua hiyo italeta mabadiliko katika jamii ya Mkoa na wakopaji kuona faida mkopo huo kwa ajili ya maendeleo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *