UNESCO:Waandishi tumieni mifumo ya Tehama katika kuandika habari za Uchunguzi.

 

Waandishi wa habari  za redio za kijamii nchini wametakiwa kutumia Mifumo ya Tehama katika kuandika na kuandaa habari za kiuchunguzi.

Hayo yamezungumwa na Marko Shekalage kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni amesema  wakati akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari yaliyofanyika katika ukumbi wa Equator Hotel uliopo Jijini Arusha.

Akizungumza kuhusu malengo ya Mafunzo hayo,Shekalage amesema kuwa yamelenga kuhakikisha wandishi wa habari za jamii wanaboresha taarifa za habari na vipindi vyao.

Shekalage ameongeza kuwa  kupitia mfumo wa tehama (ICT) wandishi wa redio jamii  watakuwa wa kisasa zaidi katika kuripoti habari zao.

Naye Mhadhiri kutoka chuo kikuu Mtakatifu Agustino (idara ya mawasiliano na habari) Peter Mataba  amesema kuwa wandishi wa habari wanatakiwa  kuibua mambo mbalimbali yaliyojificha  ili kuisaidia jamii.

Ameongeza kuwa katika kuandika habari za uchunguzi  kupitia tehama siyo lazima kuandika habari za kiuchunguzi ambazo ni mbaya, kwani kuna mambo mazuri ambayo yapo katika jamii na yanatakiwa kuibuliwa kwa kina na zenye matokeo chanya katika jamii.

Nao wanahabari walioshiriki mafunzo hayo  wamesema kuwa wandishi wa habari wengi wamejikita kuandaa habari za matukio  kwa kuhofia usalama wao huku wakiomba kuwepo na bima ambazo zitasaidia pindi watakapopata madhara.

Mafunzo hayo yametolewa kwa waandishi 27 wa redio za kijamii ziliopo Tanzania bara na visiwani Zanzibar na yameanza leo Sept 21 na yanatarajiwa kufika tamati sept 26..

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *