UN yahimizwa na miito ya kurejesha mazungumzo ya amani Libya

Umoja wa Mataifa umesema umetiwa moyo na miito ya kurejesha mazungumzo ya kumaliza mzozo nchini Libya, siku moja baada ya Misri kutangaza mpango wa amani wa upande mmoja ukiungwa mkono na wanaoegemea serikali ya upande wa mashariki mwa nchi.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umesema mapigano ya kuukamata mji mkuu Tripoli, kwa zaidi ya mwaka mmoja yamedhihirisha wazi kuwa vita yoyote miongoni mwa Walibya haitafanikiwa.

Taarifa hiyo imezihimiza pande zinazohasimiana Libya kushirikiana haraka katika mazungumzo ya kijeshi yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kufikia makubaliano ya kudumu ya kuweka chini silaha, yakifuatiwa na utekelezaji wa marufuku iliyowekwa upya na Umoja wa Mataifa ya Biashara ya Silaha.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya Walibya 16,000 wamepoteza makazi katika siku za karibuni kutokana na mapigano yanayoendelea katika mji mkuu na mji wa Tarhouna, ulioko kilometa 72, kusini mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *