Umoja wa Ulaya na Uingereza kuwasilisha matokeo ya mazungumzo yao

Umoja wa Ulaya na Uingereza hii leo watakamilisha mazungumzo yao ya awamu ya nne kuhusiana na makubaliano ya kibiashara ya baada ya Uingereza kujiondoa kutoka kwenye umoja huo.

Baadae hii leo, mjumbe wa Umoja wa Ulaya anayeratibu majadiliano ya Brexit, Michel Barnier atafanya kikao na waandishi wa habari ambapo pia Uingereza itatoa kauli yake kuhusiana na suala hilo. Awamu tatu za mazungumzo zilizopita hazikuleta matokeo yoyote makubwa kutoka pande zote mbili.

Kinachojadiliwa ni makubaliano ya biashara na ushirikiano baada ya kipindi ha mpito cha Brexit kumalizika mwishoni mwa mwaka 2020.

Uingereza ilijiondoa rasmi kutoka kwenye Umoja wa Ulaya mwishoni mwa mwezi Januari, ila bado ipo kwenye soko la ndani la umoja huo na kwenye muungano wa forodha. Iwapo hakutakuwa na makubaliano katika muda wa mwisho uliowekwa, kuna hatari ya athari mbaya za kiuchumi kutokea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *