Ujerumani kuruhusu safari katika nchi 26 za Umoja wa Ulaya

Serikali ya Ujerumani inajiandaa kuondowa tahadhari ya usafiri kwa nchi 29 za Ulaya kuanzia Juni 15 ikiwa ni karibu miezi mitatu baada ya tahadhari hizo kutangazwa kwa nia ya kuzuia kusambaa kwa kirusi cha Corona.

Uamuzi uliotolewa leo Jumatano utaimarisha matumaini ya kurudi kwa hali kiuchumi katika nchi zinazotegemea utalii ambazo zimepata athari kubwa kutokana na janga hilo la kirusi na hatua za kufungwa shughuli za kimaisha zilizotumiwa kudhibiti maambukizi.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema tahadhari za usafiri zilizowekwa kwa nchi zote duniani Machi 17 zitaondolewa nchini Ujerumani kwa nchi 26 za Umoja wa Ulaya isipokuwa kwa Uhispania ambako maafisa wameweka vizuizi dhidi ya wageni hadi Juni 21.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *