Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, William Lukuvi amezuia ujenzi usio na vibali katika maeneo yanayozunguka mji wa Dodoma.
Lukuvi ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Januari 11,2020 wakati akienda kwenye mkutano wa hadhara Mtaa wa Ndachi Kata ya Mnadani jijini Dodoma.
Lukuvi amesema suala la kujenga bila vibali halipaswi kuvumiliwa hivyo hawezi kuruhusu kazi hizo kuendelea.
“Nazuia ujenzi huu kuanzia leo, sipendi kuona shughuli zikiendelea kama hakuna vibali vya ujenzi, huwezi kujenga kama unavyotaka wewe kwa uamuzi na utashi wako, huwa hatuendi hivyo,” amesema Lukuvi.
Kiongozi hiyo alishuka kutembelea maeneo yaliyokuwa na ujenzi na akaagiza rangi maalumu ambayo huwekwa kuzuia ujenzi na ilipofika akanza.