Uingereza kuendelea kuunga mkono makubaliano ya nyuklia

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema nchi hiyo bado inaunga mkono makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani na inataka kurejea katika majadiliano baada ya mvutano wa hivi karibuni kufuatia Marekani kumuuwa jenerali wa ngazi ya juu wa Iran Qassem Soleimani.

Johnson ametoa wito wa kufikishwa mwisho uhasama, katika mazungumzo kwa njia ya simu leo na rais wa Iran Hassan Rouhani.

Alimwambia Rouhani kuwa Uingereza inaendelea kuwamo katika mpango huo wa pamoja wa kuchukua hatua, katika majadiliano yanayoendelea kuepusha kusambaa kwa silaha za kinyuklia na kupunguza hali ya wasi wasi.

Makubaliano yanayofahamika kama JCPOA yalifikiwa makubaliano mwaka 2015 baina ya Iran na mataifa matano wanachama wa kudumu katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani na Umoja wa Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *