Uganda: Sheikh ‘aliyemuoa’ mwanamume akidhani ni mwanamke asimamishwa kazi

Huku mjadala kuhusu kama kweli alifahamu jinsia ya bi harusi wake wiki mbili zilizopita alipofanya nikka naye, baraza hilo linasisitiza kuwa kuna dosari kubwa kwa upande wa imam huyo na hastahili kuendelea na kazi yake

Sheikh Mohammed Mutumba anadai kuwa alipata mshtuko wiki mbili baada ya kugundua kuwa mke aliyemuoa aliyekuwa akivalia vazi la hijab kila wakati na anafahamika kama Swabullah Nabukeera alikuwa ni mwanaume anayeitwa Richard Tumushabe.

Ukweli kuhusu jinsia yake ulibainika baada ya polisi kumkamata Tumushabe kwa madai ya wizi wa televisheni na nguo za jirani yake..

“Wakati polisi wakifanya shughuli zao za kila siku, askari wa kike alimkagua sehemu zake za mwili kabla hajampeleka jela. Na kuwashangaza maafisa wa polisi kuwa mtuhumiwa huyo kuwa aliweka nguo katika sidiria ili aonekane ana matiti,”bwana Mugera alinukuliwa.

Sheikh Mutumba – ambaye ni imam wa msikiti uliopo kijiji cha Kyampisi , kilomita takribani 100 (62 miles) kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala – alidai kuwa hajafanya naye tendo la ndoa mke wake huyo tangu amuoe kwa sababu alisema kuwa alikuwa ana matatizo ya kiafya yaliyomfanya kuendelea kupata hedhi na ilimbidi amvumilie mpenzi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *