UDSM yawataka wanahabari wanasoma Stashahada kwa njia ya Mtandao kuweka bidii ili kufikia malengo.

Kikuu cha Dar es salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari imewataka waandishi wa habari wanaosoma ngazi ya Stashahada kwa njia ya mtandao kuweka bidii katika masomo ili waweze kufikia malengo yao.

Wito huo umetolewa leo Jijini Mwanza na mratibu wa masomo ya stashahada mtandaoni kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam Dr.Darius Mukiza katika mafunzo ya namna ya kutumia elimu mtandao yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria tawi la Mwanza.

Sambamba na hayo Dr. Mukiza ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa kushirikiana na shirika la UNESCO watahakikisha wanahabari wote ambao wapo katika masomo hayo wanasoma kwa bidii na kufaulu mitihani yao na hatimaye kutunukiwa vyeti vya Stashahada baada ya kuhitimu.

Kwa upande wake mkufunzi wa njia ya elimu mtandao kutoka Chuo kikuu cha Dar es saalam Amina Kiluwasha amewataka wanafunzi kufuata taratibu za kusoma kwa njia ya mtandao na kutoa wito wa kuacha kutazama na kufuatilia mambo yasiyohusika mtandaoni wawapo masomoni.

Nao baadhi ya waandishi wa habari waliopata ufadhili huo wamelishukuru shirika la UNESCO kwa kuwalipia sehemu kubwa ya ada na kuongeza kuwa masomo hao yatawasaidia kutoondolewa kazini mwakani kwakuwa watakuwa na stashahada ya uandishi wa habari na utangazaji kutoka katika chuo kikubwa kinachotambulika.

Shirika la Elimu,Sayansi na utamaduni (UNESCO) limetoa ufadhili chini ya mradi wa SDC wa kuwalipia ada ya shilingi 525,000/=  kati ya shilingi 750,000/= kwa mwaka kwa wanahabari23  kutoka radio za kijamii nchini kusoma Stashahada ya uandishi wa habari kwa njia ya mtandao huku malengo ikiwa wanahabari 75 ambapo imebainika kuwa idadi hiyo imepungua baada ya wengine kukosa vigezo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *