Tuwe wajanja tusije tukafa kwa kukosa maarifa, mtu akikupa barakoa kataa mwambie akavae na mkewe- JPM

“Watu watakuja Kuwaambia Mvae, Watanzania tujifunze kuelewa. Anapokuletea Mtu Barakoa na haujui hata ameitoa wapi kataa mwambie akavae yeye na mke wake na watoto wake Nyumbani kwake TUTAUMIZWA

Tuwe wajanja tusije tukafa kwa kukosa maarifa” – Rais MAGUFULI

“Ukitaka kuvaa barakoa kashone yako, mbona ni rahisi tu, barakoa mbona imekaa kama titi moja la Mtu mmoja hivi limekatwa upande mmoja, weka huku kama… aaah samahani Mh.Waziri nimesema hapa, nilikuwa nachomekea tu kidogo” -JPM

“Juzi nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari kuna group linaitwa Magufuli Forum wala silijui, ila sishangai Mtu kujiita Magufuli hata akijiita fisi ni hiyari yake, lakini walikuwa wanagawa barakoa wala hazijulikani zinatoka wapi, tutaumia kwa kukosa maarifa”-JPM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *