Tundu Lissu Kutumia Zao la Chai, Mbao Kuinua Uchumi

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kutokana na utajiri mkubwa uliopo katika mkoa wa Iringa unaotokana na mbao na chai, ulitakiwa uwe kitovu cha viwanda vya kutengeneza samani katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Alisema akichagulia kuwa rais, atahakikisha anabadilisha utajiri wa rasilimali zilizopo katika mkoa huo za mbao na chai kunyanyua uchumi wa mkoa huo.

Lissu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia katika kampeni katika maeneo ya Mufindi Kaskazini na Mafinga mkoani humo.

Lissu alisema akichaguliwa kuwa Rais, atahakikisha kwamba anatumia rasilimali zilizopo katika mkoa huo kuinua uchumi katika mkoa huo na kumaliza changamoto zote zilizopo kwa sasa.

Pia alisema ataondoa kodi zote ambazo wakulima wa miti na chai wamekuwa wakitozwa ili wanufaike na kilimo cha mazao yao katika kuwaletea maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *