Trump kutoa tamko dhidi ya shambulizi la iran

Kambi mbili za Jeshi la Marekani nchini Iraq zimeshambuliwa kwa makombora kadhaa huku Television ya kitaifa ya Iran ikitangaza kuwa shambulio hilo ni la kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya Qassem Soleimani aliyeuawa na Marekani katika shambulio la Drones Iraq.

Rais Donald Trump amethibitisha kutokea kwa shambulio hilo katika mbi zao mbili zilizopo Iraq na amesema wanafanya tathimini ya waliopata madhala au uhalibifu wa mali ndipo atatoa tamko.

“Kila kitu kipo sawa, Kambi zetu mbili za Jeshi la Marekani zilizopo Iraq zimeshambuliwa na Iran, tunafanya tathmini kujua kama kuna waliopata madhara au uharibifu wowote wa mali, yote kwa yote tuna vifaa Bora vya kivita kuliko Nchi yoyote Duniani, nitatoa tamko hivi punde” -Donald Trump, Rais wa Marekani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *