Trump, Biden “wafanya mdahalo” kwa vituo tafauti vya TV

Wagombea wakuu wa urais nchini Marekani, Donald Trump wa Republican na Joe Biden wa Democratic, wamejitokeza katika vituo viwili tafauti vya televisheni, kila mmoja akimtuhumu mwenzake, juu ya namna anavyouchukulia ugonjwa wa COVID-19.

Akihojiwa na kituo cha televisheni cha NBC mjini Miami, Trump alikataa kusema waziwazi, endapo wakati wa mdahalo wake wa kwanza na Biden, alipimwa na kugundulika kutokuwa na virusi vya corona.

Trump, aliuguwa ugonjwa huo siku chache baada ya mdahalo huo, wa tarehe 29 Septemba, na kupelekea kulazwa hospitalini. Kwa upande wake, Biden alihojiwa na kituo cha televisheni cha ABC, mjini Phila-delphia, ambapo alisema Trump hajayachukulia maradhi hayo, yashayoangamiza Wamarekani zaidi ya 210,000, kwa umakini zaidi.

Trump alikataa kushiriki mdalaho mwengine na Biden kwa njia ya mtandao, baada ya waandaaji kuufuta mdahalo wa moja kwa moja, kutokana na yeye kuuguwa COVID-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *