Tito Magoti na mwenzie wafikishwa Mahakamani tena leo

Afisa Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti (26) na mwenzake ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Tehama, Theodory Gyan (36), wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kesi yao ya utakatishaji fedha wa zaidi ya Sh. Milioni 10.

Magoti na mwenzake walifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon akisaidiana na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, Faraja Nchimbi na Renatus Mkude.

Miongoni mwa mashitaka yao wanadaiwa Februari mosi, 2019 na Desemba 17, 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam kwa pamoja washtakiwa mengine ambao hawapo mahakamani walimiliki programu ya kompyuta iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kutenda makosa ya jinai.

Washtakiwa hao wanasota korokoroni kwa sababu kesi yao ya uhujumu uchumi na haina dhamana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *