Meghan Trump na Biden wafanya kampeni za ´lala salama´

Rais Donald Trump wa Marekani na mpinzani wake kutoka chama cha Democratic Joe Biden wamefanya mikutano kwenye majimbo yenye ushindani mkali kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais kesho Novemba 3.
Akizungumza kwenye jimbo lenye mchauano mkali la Michagan, Trump amewaonya wafuasi wake kuwa Biden atazifunga shughuli za kawaida kama njia ya kukabiliana na janga la virusi vya corona, mbinu ambayo Trump anadai inavuruga uchumi.

Kwa upande wake Biden aliyehutubia mjini Philadelphia amerejea matashi yake ya kumshambulia rais Trump kwa jinsi anavyoshughulikia janga la virusi vya corona ambalo limesabaisha vifo vya zaidi ya watu 230,000 nchini Marekani.

Wagombea wote wanatumia siku za mwisho za kampeni kufafanua misingi ya sera na ilani huku kura za maoni ya umma zikionesha Joe Biden anaongoza dhidi ya Trump anayewania muhula wa pili kwenye uchaguzi huo wenye ushindani mkali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *