Tetesi za soka Ulaya leo Juni 5

Beki wa kushoto wa England Ben Chilwell 23, anashawishiwa na kujiunga na Chelsea baadae msimu huu lakini bado hajaomba kuondoka Leicester City . (Mirror)

Liverpool haitapambana na Chelsea kwa ajili ya kupata sahihi ya Timo Werner wakati mshambuliaji huyo,24, anayekipiga RB Leipzig yuko kwenye mpango wa kuelekea Stamford Bridge. (Evening Standard)

Tottenham wanamsubiri mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Jan Vertonghen,33, kuamua kama ataendelea kubaki mpaka msimu utakapomalizika au ataondoka kabla msimu kuisha (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Newcastle Matty Longstaff hajakuwa mazoezini wiki hii wakati kukiwa hakuna uhakika kuhusu mustakabali wake kwenye klabu hiyo, huku klabu ya Udinese ya Serie A ikiripotiwa kutoa ofay a mshahara wa pauni 30,000 kwa wiki kwa mchezaji huyo, 20, ambaye mkataba wake utakwisha msimu huu. (Mail)

Manchester City wanatarajia kuanza mazungumzo na mchezaji wa nafasi ya ulinzi Mhispania Eric Garcia huku klabu yake ya zamani Barcelona ikimtaka mchezaji huyo. (Mail)

Manchester United wanajiandaa kutoa mkataba mpya kwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi Brandon Williams ukiwa na marekebisho katika mshahara wake wa sasa wa pauni 40,000 kwa wiki, baada ya kufanya kazi nzuri msimu huu. (Athletic)

Arsenal wanaweza kuwa tayari kumuuza mchezaji wa nafasi ya ulinzi Kieran Tierney,23, kwa Leicester City, miezi 12 tu baada ya kuhamia Emirate(Express)

Kocha wa England Gareth Southgate hatahudhuria michezo ya ligi ya primia msimu utakapoanza kwa kuwa anahisi kuwa uwepo wake kwenye viwanja hauna umuhimu. (Star)

Real Madrid wanapendelea kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho,20. (AS)
Juventus imewasiliana na Barcelona kwa lengo la kusaini mkataba na mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele, mwenye umri wa miaka 23, kwa mkopo msimu huu. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Matumaini ya kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kuongeza kitita kwa ajili ya uhamisho kupitia mauzo ya wachezaji kama Marcos Roho, 30 , Beki wa kati Chris Smalling na mshambuliaji Alex Sanchez, 31, watakumbwa na athari zilizotokana na janga la virusi vya corona (Evening Standard

Ryan Fraser wa Bournemouth anayejiandaa kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu, anaweza kuwa mmoja kati ya wachezaji wanaohitajika sana kwenye ligi. (The

Paris St-Germain wanahitaji pauni milioni 156 kutoka Barcelona kwa ajili ya mshambuliaji wa Kibrazil Neymar, 28. (Sport in Spanish)

Watazamaji watakuwa na nafasi ya kusikiliza kelele za kutengeneza za mashabiki wakati Ligi ya Primia itakaporejea. (Mirror)

Barcelona ina mpango wa kumsaini tena beki wa kati wa Kihispania Eric Garcia,19, kutoka Manchester City. (ESPN)

Arsenal wako tayari kumpatia mchezaji wa nafasi ya ulinzi David Luiz, 33, mkataba wa mwaka mmoja lakini watapunguza mshahara wake wa wiki (Mirror)

Manchester United wamebainisha kuwa winga wa Velez Sarsfield Thiago Almada,19, anawezekana akawa sehemu ya mpango wao wa uhamisho mbadala wa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20. (Manchester Evening New

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *