Tetesi za soka kimataifa

Manchester United wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kutoka Barcelona. (Daily Record)
Vyanzo vingine kutoka United vimepuuza kuhusishwa huko na Dembele. (Mirror)

Paris St-Germain wana uhakika kwamba kiungo wa Tottenham Hotspur na England Dele Alli, 24, anataka kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa msimu mzima. (Mail)

Mlinzi wa Norwich City Muingereza Max Aarons (20) amekubali mkataba wa miaka mitano kujiunga na Barcelona. (Sport – in Spanish)

Kiungo wa Klabu ya Arsenal na Ufaransa Matteo Guendouzi, 21, ameomba kuondoka klabuni hapo. (Tribal Football)

Borussia Dortmund wana uhakika winga wa England Jadon Sancho, 20, hataondoka kwenye klabu hiyo msimu huu wa usajili, licha ya kuhusishwa na Manchester United. (Independent)

Newcastle United wanamtaka mshambuliaji wa Napoli na Poland, Arkadiusz Milik, 26. (Corriere dello Sport – in Italian)

Southampton wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati raia wa England Tom Davies kutoka Everton. (Talksport)

Arsenal imepata mpinzani wa klabu inayoshiriki ligi ya mabingwa Ulaya, katika mbio zake za kumwania kiungo wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar, 22. (Telegraph – subscription required)

Mlinzi wa Chelsea mjerumani Antonio Rudiger, 27, anaangalia hatma yake klabuni hapo baada ya kuachwa kwenye kikosi cha kwanza. (Sky Sports)

Mlinzi wa Bayer Leverkusen, mjerumani Jonathan Tah, 24, hayuko kwenye orodha muhimu ya wachezaji wanaowaniwa na Leicester City.(Kicker – in German)

Fulham wanajaribu kumsajili kwa mkopo winga wa zamani wa Everton na Charlton Ademola Lookman. Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa sasa anachezea RB Leipzig. (Evening Standard)

Kiungo wa Manchester United na England Jesse Lingard, 27, hatajiunga na Tottenham licha ya kuhusishwa kwake kutaka kuhamia timu hiyo. (Athletic – via Twitter)

Mashetani wekundu The Red Devils kumuongezea mkataba wa hadi mwaka mmoja Lingard ili kutunza thamani yake ya £25m. (Sun)

Winga wa Southampton, raia wa Morocco Sofiane Boufal, 27, anawaniwa na klabu ya Ufaransa ya Angers. (L’Equipe, via Daily Echo)

Winga wa Wales Daniel James, 22, huenda asiondoke Manchester United msimu huu, licha ya kuhusishwa na Leeds United. (Manchester Evening News)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *