TCRA Kanda ya ziwa imewataka wananchi kuzitumia vizuri siku 20 zilizoongezwa na Rais Magufuli kusajili laini zao.

Jamii imetakiwa kutumia siku 20 zilizoongezwa na rais JOHN POMBE MAGUFULI kusajili laini zao kwa alama za vidole ili kuepusha usumbufu wa kukosa mawasiliano baada ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima laini zote ambazo zitakua hazijasajiliiwa.

Hayo yamesemwa leo na mkuu wa kanda ya ziwa  kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) FRANSIC MIHAYO katika kipindi cha Ukurasa mpya kinachorushwa na kahama fm.

Amesema ni muhimu wananchi kusajili laini zao ili kuwalinda watumiaji dhidi ya matumizi mabaya ya laini, kuwawezesha watumiaji kutambuliwa ili kuongeza thamani na kuimarisha usalama wa Mtumiaji na watu wengine katika jamii.

Amesema wapo baadhi ya watu ambao hawana utaratibu wa kufuatilia vitambulisho vyao na kuendelea kulalamika kwamba wanashindwa kusajili laini kutokana na kukosa vitambulisho huku tayari vitambulisho au namba zao tayari zipo.

Kuhusu waandishi wa habari kuwa na elimu kuanzia DImploma na kuendelea amesema sheria ilipitishwa na bunge na inachofanya sasa TCRA ni kuwakumbusha kuwa kufikia tar 31 december 2020 itakua ni mwisho kufanya kazi za uandishi na utangazaji katika chombo chochote cha habari nchini.

Ikumbukwe kuwa Taarifa iliyotolewa  desember 27, mwaka huu na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu, imeeleza Rais MAGUFULI ameongeza siku 20 kuanzia Januari Mosi hadi 20, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia Desemba 31, mwaka huu,  kama ilivyotangazwa na TCRA.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *