TAMWA Zanzibar yatimiza miaka miatano, Mkurgenzi mtendaji ataja mafanikio ndani ya kipindi hicho

Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari TAMWA-ZNZ Dkt, Mzuri Issa amaesema kuna mafanikio makubwa ya kiutendaji ndani ya Chama hicho kwa miaka mitano iliopita kutoka mwaka 2016 mpaka 2020.

Aliyasema hayo katika ofisi za Chama hicho zilizopo Tunguu wilaya ya kati Unguja wakati akitoa taarifa za kiutendaji kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho na wadau kutoka katika taasisi mbali mbali ndani ya ukumbi wa chama hicho uliopo Tunguu wilaya ya kati Unguja.

Alisema wajumbe hao  wakati wanaendelea kujadili mkakati mwengine mpya wa kiutendaji ndani ya chama hicho wanapaswa kufahamu kuwa chama chao kimefikia malengo zaidi ya asilimia tisini waliojipangia.

Akitaja baadhi ya mafanikio hayo Dkt,Mzuri alisema ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi hususani vijijini katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba ambapo jumla ya wanufaika walikua ni 6872.
Alisema jitihaza za kuwawezesha kiuchumi wanawake hao imekua  chanzo  cha kuwa kwamua wanawake hao kiuchumi na wamekua tegemea kubwa kwa familia zao tofauti na ilivokua.

Akiendelea kueleza zaidi baadhi ya mafanikio mengine ni uwepo wa vikundi mbali mbali vya kuweka na kukopa ambapo hadi miaka mitano ya utekelezaji inamalizika kiasi cha shilingi bilioni 1.5 zimeweza kuwekwa kwenye vikundi hivyo na wanachama wanaendelea kukopeshana.

Alisema hayo yote yamekuja kutokana na uhamasishaji bora uliofanywa na chama hicho kwani hapo awali wanawake wengi hawakuwa na uelewa wa kuanzisha vikundi wala kuweka hakiba zao.

‘’Kwa mazingira haya wapo akinamama wengi walionyanyaswa na waume zao na kuonekana kama mzigo lakini sasa wamekua watu huru na mashujaa hata waume zao wanawaunga mkono’’aliongeza.

Katika Nyanja za kisiasa Mzuri alisema wameweza kuwaandaa wanaume wa mabadiliko 20 kutoka Unguja na Pemba ambao walikua na kazi kubwa ya kujenga ushawishi ili jamii iwe na ufahamu mkubwa na kuona umuhimu wa kuwapa nafasi za uongozi wanawake.

Alisema kuna mafanikio makubwa katika mkakati huo  na kwamba tayari wamewajengea uwezo jumla ya wanawake wapatao 4071 kutoka katika wadi 55 ambapo Unguja 32 na Pemba 23.

Alieleza kuwa awali kabla ya mkakati huo wanawake wengi Zanzibar walikua wakishindwa kujieleza hadharani na ndio maana kwa muda mrefu viongozi wengi waliendelea kubaki kuwa wanaume hususani katika nafasi za kuchaguliwa majimboni.

Mkurugenzi huyo  anaamini kuwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika  mwezi oktoba mwaka huu ana matumaini makubwa kuwa wanawake wengi watajitokeza na kupewa fursa za uongozi kwenye vyama vyao.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi na viongozi wa vyama vya siasa kuhakisha wanawaunga mkono na kuthamini jitahada za kila mwanamke atakaejitokeza kugombea.

Kuhusu mapambano dhidi ya matendo ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto alisema kuwa kesi za udhalilishaji kwa wanawake na watoto zinaendelea kushamiri sikua hadi siku visiwani hapa waliamua kuongeza nguvu zaidi ikiwmeo kujitoa na kuwajengea uwezo wananchi waweze kufahamu madhara ya matendo hayo.

Alisema mkakati huo ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo jumla ya watu 26927 walipatiwa elimu ya kutosha katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.

Alieleza kuwa baada ya kujengewa uwezo wananchi hao hivi sasa kumekuwepo na muamko mkubwa kwa wananchi kuripoti matukio ya udhalilishaji yanapotokea na kwa haraka zaidi.

Huku hayo yakijiri alisema jumla ya matukio ya udhalilishaji (11120) yamechukuliwa hatua  mbali mbali na kesi 280 zinaendelea na ufuatiliaji huku kesi 182 zinaendelea na upelelezi katika vituo vya polisi.

Aidha Dkt,Mzuri akiendelea kufafanya zaidi alisema kesi (76) zimekwisha na kesi (16) zimeshatolewa hukumu na kesi 91 zipo katika ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DDP na (39)zipo katika Mahakama mbali mbali Unguja na Pemba.

Sambamba na hayo akiendelea kubainisha mafanikio mengine alisema ni pamoja na kutengeneza mitandao ya kupambana na udhalilishaji  katika wilaya tano ambapo Unguja ni wilaya tatu na Pemba wilaya mbili.

Akitaja wilaya hizo ni pamoja na wilaya hizo kwa upande wa Unguja ni wilaya ya kusini,kaskazini na magharibu huku kwa upande wa Pemba ni wilaya ya Mkoani na wilaya ya Wete.

Alieleza kuwa kupitia mitandao hayo kumeleta faraja kubwa kwa kuwa wamekua wakifanya kazi kwa ukaribu mkubwa na Chama hicho hususani katika matukio mbali mbali ya kupambana na udhalilishaji kwa kijinsia.

Alisema licha ya uwepo wa mafanikio makubwa ya kiutendaji ndnai ya chama  hicho lakini pia kumekuwepo na changamoto za hapa na pale.

Akitaja baadhi ya changamoto ni pamoja na wajasiriamali kutozalisha bidhaa zao kwa wakati ambazo anaamini zingeweza kuleta tija zaidi.

Alieleza kwa kuwa kuna mazingira ya aina hio hadi sasa bado akinamama hao hawajasimama ipasavyo kuwa wajasiriamali wenye kutajika na kujingizia kipato zaidi.

‘’Ninaamini iwapo mabadiliko zaidi sambamba na utayari yatafanyika na kila mmoja wetu jamii inaweza kubadilika na kupiga hatua zaidi kimaendelea hatimae maslahi mapana kwa Taida zima yanaweza kupatikana’’aliongezea.

Aliesema licha ya kuwepo kwa mafanikio makubwa kwa kipindi kilichopita lakini bado wanaendelea kufikri zaidi ikiwemo kuangazia Nyanja zote ambazo hawakuzigusa au walishindwa kufanya vizuri.

Akitolea mfano ni pamoja na matumizi ya teknolojia kwa watendaji na wanachama wa chama hicho ambavyo anaamini kuwawezesha wanachama wao ni kuawezesha wengine walio wengi zaidi.

Raya Hamad ni mmoja miongoni mwa wanachama,anasema ipo haja kubwa kuzingatiwa zaidi maoni ya wanachama katika utelekezaji wa mkakati mpya wa miaka mitano ijayo.

Alisema wanachama wamekua wakikabiliwa na changamoto mbali mbali hususani kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea kukua kila leo.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya chama hicho alisema ipo haja kwa Tamwa kuwa na kitengo maalumu cha utafiti ambacho kitafanya kazi kwa umakini mkubwa na kugundua changamoto mbali mbali kwa njia ya utafiti.

Alisema kuwepi kwa kitengi hicho kutasaidia kwa kiasi kikubwa utendaji wa kazi wa chama na kupunguza gharama sambamba na kupata takwimu sahihi za matukio mbali mbali ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto sambamba na kueleza hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Kwa upande wake mtalamu wa maswala ya kutengeneza mkakati ambae pia ni wakili Clarence Kipobota alisema mpango mkakati katika taasisi yoyote hile ni jambo muhimu na lenye kuzingatiwa.

Alisema kuwepo kwa mpango mkakati kunapelekea watendaji wa taasisi husika kufanya majukumu yao kwa umakini mkubwa bila ya kutoka kwenye matarijio yao.

Alishauri taasisi nyengine kujiwekea utaratibu huo kwa kuwa pia hujenga uaminifu kwa jamii pamoja na wafadhili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *