TAKUKURU yaonya vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi serikali za Mitaa

Kuelekea katika uchaguzi wa serikali za Mitaa utakaofanyika jumapili hii novemba 24, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, Mkoani Dodoma imewanya watu kutojihusisha na vitendo vya Rushwa kwani taasisi hiyo imejipanga kikamilifu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Mkuu wa taasisi ya TAKUKURU, Mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo, amesema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanakabiliana na vitendo hivyo.

“Serikali imetuwezesha kwahiyo tupo kamili kakabiliana na vitendo hivyo na tunawataka wananchi kutojihusisha na vitendo hivyo kwenye uchaguzi huu na wananchi wahakikishe wanachagua watu wasiokuwa watoa Rushwa” amesema Kibwengo.

Katika hatua nyingine amesema wamewanasa na inawashikilia viongozi wa chama Cha ushirika Cha akiba na mikopo Cha matumaini(Matumaini SACCOS) kilichopo kata ya Msanga Wilayani Chamwino kwa kosa la matumizi mabaya ya Mamlaka.

“Uchunguzi wetu unaonesha kuwa watuhumiwa hao bwana Charles Chilongani(51) ambaye alikuwa ni Meneja, Bw. Isaya Kigalika (54) mhasibu na bi Mwanahamis Kaisi(33) ambaye ni karani karani wa SACCOS hiyo wote wakazi wa Chamwino” amesema.

Amesema Kati ya mwaka 2011 na 2013 kwa pamoja walichakata bila kupata idhini ya mrajisi wa vyama vya ushirika na kuwezesha SACCOS hiyo kupata bila kustahili mkopo wa shilingi milioni Mia moja arobaini na nane(148,000,000) kutoka benki ya uwekezaji Tanzania (TIB) kinyume na matakwa ya kisheria ya vyama vya ushirika.

Aidha amesema TAKUKURU kwa kushirikisha na Ofisi ya mwendesha mashitaka mkoa wa Dodoma, wamemfikisha inatarajia kumfikisha mahakamani bwa.Ibrahim Kahogo, (43) mkazi wa area A Jijini Dodoma kwa kosa la kughushi na kujifanya mwingine na kutoa taarifa za uongo kwa mtu aliyeajiliwa Katika utumishi wa Umma na kutoa nyaraka za uongo.

Amesema mwaka 2019 mtuhumiwa akiwa akiwa katika Ofisi ya kamishna wa kazi Jijini Dodoma alitumia njia ya kudanganya ili kumuwezesha kuomba na kuchukua vibali vya kufanya kazi kwa wageni ambao wameajiriwa na taasisi ya one Acre Fund ya Mjini Iringa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *