TADIO:Redio za kijamii Tumieni Redio zenu kutatua changamoto za wananchi katika maeneo yanayowazunguka.

MWANZA
Mtandao wa redi za kijamii Tanzania(TADIO) umezitaka redio za kijamii nchini kutumia redio zao kutatua changamoto za wananchi zilizopo katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa leo jijini Mwanza na mratibu wa mafunzo ya habari za kudumisha Amani kutoka TADIO Cosmas Lupoja wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa redio 34 za kijamii kutoka Tanzania bara na Zanzibar.

Lupohja amesema kuwa TADIO kwa muda mrefu imejikita katika kutafuta matangazo ya biashara ili kuzisaidia kiuchumi redio washirika wa mtandao huo na kwamba kwa sasa wanajipanga kuzitumia redio hizo kujikita katika kuandaa vipindi vya kuzisaidia jamii katika Nyanja mbalimbali.

Lupoja ameongeza kuwa TADIO ipo pamoja na redio za kijamii katika kuleta maendeleo ya wananchi kupitia redio hizo na kuwataka mameneja kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu vituo vyao ili kuleta ufanisi wa utendaji kazi wa kila siku.

Nao wenye viti wa madarasa ya mafunzo hayo Elias Maganga kutoka Pambazuko Fm Ifakara Morogoro na Edwin Mpokasye kutoka Fadhila Fm ya Masasi Mtwara wameushukuru mtandao huo kwa kuwapa mafunzo hayo na kuomba yazidi kutolewa ili kuwaimarisha waandishi katika habari za kuhamasisha Amani na kuwa wazalendo kwa nchi yao.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Chevawe Mandari kutoka HUHESO Fm na Daniel Manyanga kutoka Sibuka Fm wameshukuru kupata mafunzo hayo na kwamba yatawasaidia katika kuandaa vipindi bora vitakavyoleta Amani na maendeleo katika maeneo hayo.
Mafunzo hayo siku tano yameshirikisha washiriki sabini kutoka Redio thelathini na nne za bara na visiwani pamoja na chama cha waandishi wa habari Pemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *