Siku za Unai Emery zahesabika, Mourinho kutua Arsenal

Kocha wa klabu ya Arsenal, Unai Emery amepewa mwezi mmoja wa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri, hii ni kufuatia matokeo ya sio ridhisha ambayo imekuwa ikiyapata huku taarifa za ndani zikidai kuwa Jose Mourinho ndiye anayetarajiwa kuja kurithi nafasi yake.

Taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa, Unai Emry atatimuliwa kazi msimu huu kama timu hiyo haitakuwa kwenye kiwango bora na tayari mipango imeanza ya kutaka kumpata mrithi wake.

Katika kuhakikisha Arsenal inakuwa kwenye nafasi nne za juu kunako msimamo wa ligi kuu England ili kujikatia tiketi ya kushiriki michuano ya Champions League, Bosi wa ‘the gunners’ ambaye ndiyo mwenye mamlaka ya kusimamia soka, Raul Sanllehi inadaiwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mreno Jose Mourinho kimya kimya wakati alipomualika kwenye chakula cha usiku.

Hata hivyo taarifa hizo zikipingwa vikali na kudaiwa wawili hao hawajapata nafasi ya kukutana kwa muda mrefu sasa.

Inaaminika kuwa kutua kwa Mourinho ndani ya Arsenal ni rahisi kwa klabu hiyo kutwaa mataji kama alivyopata kufanya kwenye timu ambazo amewahi kuzitumikia zikiwemo Chelsea ambapo aliipatia makombe matatu na hata alipokuwa Manchester United.

Mpaka sasa Arsenal imepoteza jumla ya michezo miwili, sare tano ikiwa nafasi ya tano huku ikisaliwa na jumla ya mechi 27 kunakonPremier League hivyo wanayo nafasi ya kufanya vizuri.

Baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Wolves siku ya Jumapili, Emery amesema yeye ndiyo anayepaswa kutupiwa lama.

Mourinho amekuwa nje ya majukumu ya soka tangu mwezi Desemba mwaka jana baada ya kutimuliwa kazi na Manchester United last December.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *