Serikali yatoa angalizo kuelekea dabi ya Kariakoo

Serikali imesema imejiandaa kukabiliana na mianya yote ya upigaji iliyokuwa ikiwanufaisha wachache na kusababisha Serikali kukosa mapato stahiki katika tozo rasmi ya malipo halali ya viingilio viwanjani.

Katibu mkuu  wa wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt. Hassan Abbas amesema, kuelekea mchezo wa watani sambamba na mchezo wa kimataifa wa kirafiki Oktoba 11, kati ya Tanzania na Burundi serikali imejiandaa kudhibiti mianya yote ya upigaji.

“Tumeshaanzisha mfumo wa kielekroniki na hatutaki kusikia wananchi wakilalamikia usumbufu wa kuingia viwanjani kwani huu mfumo mpya wa N-card unamuwezesha mwananchi kununua tiketi kupitia simu janja yake lakini pia tunaenda kuboresha mfumo wetu pia kuwawezesha wenye simu za kawaida kuweza kunufaika na huduma hii baada ya wiki mitandao yote itakuwa inatoa huduma hii”, amesema Abbas.

Aidha, Dkt. Abbas ameongeza lengo la mfumo huu maalumu ni kwaajili ya kuwawezesha wananchi kuepuka usumbufu ambao umekuwa kikwazo kwa wanachi wengi kuingia viwanjani lakini pia selikali imekuwa ikipoteza mapato mengi kutokana na mianya inayotumiwa na raia wasiowaaminifu.

”Ukweli ni kuwa serikali inawekeza kiasi kikubwa cha fedha kuhudumia uwanja na usalama wa watu viwanjani la muhimu mashabiki wanatakiwa kuzingatia uingiaji viwanjani kwa heshima kwakuwa serikali”, ameongeza Dkt. Abbas.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *