Serikali yaridhishwa na usalama na mazingira ya wanafunzi wa Kidato cha sita nchini

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo aridhishwa na usalama na mazingira ya wanafunzi wa kidato cha sita waliofungua shule mara baada ya Serikali kutangaza kufungua vyuo na shule za Sekondari nchini.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea shule za Sekondari za Ihungo na Rugambwa kukagua na kujiridhisha na usalama wa wanafunzi siku chache baada ya Serikali kufungua kutokana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Korona.

Amesema kuwa Serikalli imejipanga kuhakikisha mazingira yanaimarishwa hasa katika suala zima la ugonjwa wa Korona ili kupunguza maambukinzi nchini.

Mhe Jafo amewataka wanafukunzi kutokuwa na hofu bali wajitahidi katika masomo yao na kuwatakia maandalizi mema katika kujiandaa na mitihani ya kidato cha Sita Mwaka huu
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Rugambwa Bi.Kagemulo Lupanka amesema kuwa wanafunzi 173 kati 175 wa kidato cha sita wameripoti shule na wanafunzi wawili hawajaripoti kutokana na ugonjwa kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na wazazi.

Amesema kuwa kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali ya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya korona shule imeandaa mazingira wezeshi kwa wanafunzi kujifunza.

Aidha, Ikumbukwe kuwa Serikali ilitangaza kufunga shule zote na vyuo vya juu mnamo mwezi wa Aprili, 2020 kutokana na kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa Korona nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *